المدة الزمنية 14:12

JWTZ: Hakuna Nafasi ya Kuingizwa Jeshini kwa Kutumia Mgongo wa Fedha

بواسطة The Chanzo
1 094 مشاهدة
0
8
تم نشره في 2021/11/30

Baada ya kutangazwa kwa nafasi za usahili kwa vijana walioko kwenye makambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wenye sifa za kujiunga na Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kumeibuka tabia, mwenendo na vitendo vya baadhi vya watu ambao wameanza kutumia fursa hiyo ya uandikishwaji wa vijana kujinufaisha ikihusisha vitendo vya rushwa na ulaghai kwa wananchi watoe fedha ili vijana wao wapate nafasi hizo. Kutokana na hali hiyo Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kupitia Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano Jeshini Luteni Kanali Gaudence Gervas Ilonda limetoa ufafanuzi juu ya zoezi hilo la usahili linaloendelea kwa kueleza kuwa “hakuna nafasi ya kuingizwa jeshini kwa kutumia mgongo wa fedha”. #TheChanzo

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 0