المدة الزمنية 29:15

LIVE: WAZIRI UMMY MWALIMU AKITANGAZA NAFASI ZA AJIRA.

بواسطة Millard Ayo
36 015 مشاهدة
0
352
تم نشره في 2021/05/09

OFISI ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), imepata kibali cha ajira za walimu wa shule ya msingi na sekondari 6,949 na kada mbalimbali za afya 2,726 watakaoajiriwa chini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini. Maombi ya ajira hizo yataombwa kwa njia ya mtandao kuanzia Mei 9 hadi 23, mwaka huu kupitia kiunganishi cha ajira.tamisemi.go.tz. Akizungumza na waandishi wa habari leo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Ummy Mwalimu, amesema ajira hizo zitajaza nafasi zilizoachwa wazi na watumishi waliokoma utumishi kutokana na sababu mbalimbali. “Serikali imetoa kibali, maana mara baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kueleza kwamba atatoa ajira 6000 kwa walimu tulikuwa tunapata msukumo mkubwa kutoka kwa wananchi wakihoji kwanini TAMISEMI hatutangazi, taratibu za serikali lazima tupate kibali Menejimenti ya Utumishi wa umma,”amesema. Hata hivyo, amesema serikali imetoa fursa kwa waombaji ambao ni walemavu kutuma maombi yao kwa nakala ngumu na yaeleze aina ya ulemavu wao na picha zao na kutumwa kwa anuani ya Katibu Mkuu TAMISEMI na Ofisi ya Waziri Mkuu ili aione Mkurugenzi wa kitengo cha watu wenye ulemavu. Akitaja sifa za waombaji wa ualimu, Waziri Ummy amesema kwa shule ya msingi wanatakiwa walimu wenye daraja la IIIA kuwa astashahada ya elimu ya msingi, elimu ya michezo, elimu ya awali na elimu maalum. “Mwalimu wa daraja la IIIB anatakiwa kuwa mhitimu wa stashahada ya ualimu wa elimu ya awali, msingi, elimu maalum na Mwalimu wa daraja la IIIC, mhitimu wa shahada ya ualimu masomo ya lugha ya kiingereza, historia na jiografia

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 84